Wataalamu watarajia AfCFTA itasaidia ukuaji jumuishi barani Afrika
2024-05-28 14:37:12| cri

Wataalamu barani Afrika wamesema utekelezaji kamili wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) utachochea ukuaji jumuishi katika bara hilo.

Wakizungumza katika mkutano wa 59 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) mjini Nairobi, Kenya, wataalamu hao wamesema kuongezeka kwa biashara katika bara hilo kutapunguza utegemezi wa Afrika katika masoko ya jadi ya Magharibi.

Katibu Mkuu wa Kundi la AfDB Vincent Nmehielle amesema, kutoa uhuru wa biashara barani Afrika kwa kuondoa ushuru wa kuagiza bidhaa zinazozalishwa ndani ya bara hilo kutaboresha maingiliano ya kibiashara katika bara hilo na kunufaisha wafanyabiashara wadogo.

Eneo la Biashara Huria la Afrika, linalokadiriwa kuwa na watu bilioni 1.2, linatarajiwa kutoa manufaa mengi ya kijamii na kukabiliana na ukosefu wa usawa wa Afrika kwa kuwezesha jamii zilizotengwa.