Kikao cha 77 cha Baraza la Afya Duniani chafunguliwa Genava
2024-05-28 09:14:30| CRI

Kikao cha 77 cha Baraza la Afya Duniani (WHA) kilifunguliwa jana mjini Geneva, Uswisi, kikiwa na kauli mbinu ya “Kila Kitu Kwa ajili ya Afya, Kila Mtu Awe na Afya.”

Katika kikao kicho cha siku sita, wajumbe wa WHA watapitisha mpango mkuu wa 14 wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ambao utakuwa ni mkakati mkuu wa WHO kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2025 hadi 2028, na unalenga kukabiliana na athari za masuala ya mabadiliko ya tabianchi, kuzeeka kwa idadi ya watu, uhamiaji na maendeleo ya teknolojia kwa afya na maslahi ya watu. Wajumbe wanaoshiriki kwenye kikao hicho pia watajadili kuhusu utungaji rasimu ya Mkataba wa Mlipuko Mkubwa wa Magonjwa na marekebisho ya Kanuni za Afya za Kimataifa, na kutoa maamuzi kwa masuala ya vipaumbele, ikiwemo tabianchi na afya, kazi ya WHO katika matukio ya dharura ya kiafya, maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, afya ya akili, afya ya wanawake na mageuzi ya WHO.