Tanzania kuimarisha hatua za usalama katika eneo la Maziwa Makuu
2024-05-29 09:22:43| CRI

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) jana Jumanne lilitangaza mipango ya kutekeleza hatua za ziada za ulinzi na usalama katika eneo la Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika, Nyasa na Rukwa.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Mohamed Salum amesema kuwa mradi husika umeanzishwa katika Ziwa Victoria, ukihusisha kuimarisha mawasiliano kupitia simu za mkononi, kujenga vituo vitatu vidogo vya utafutaji na uokoaji majini pamoja na kituo kimoja cha kikanda cha uratibu wa uokoaji, pia itashirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Tanzania kuboresha mfumo wa utabiri wa hali ya hewa kwa kuweka maboya mawili ya hali ya hewa katika ziwa hilo. Licha ya hayo, mradi huo pia utanunua boti mbili za utafutaji na uokoaji na boti moja ya ambulensi ili kutoa huduma za afya kwa watumiaji wa ziwa haswa katika maeneo yasiyo na vituo vya matibabu, kama vile visiwani.