China yatoa ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Marekani mwaka 2023
2024-05-29 13:28:46| cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China Jumatano ilitoa Ripoti kuhusu Ukiukwaji wa Haki za Binadamu nchini Marekani mwaka 2023, ikifichua hali inayozorota ya haki za binadamu nchini humo kwa kutumia ukweli na takwimu.

Ripoti hiyo inaitaka serikali ya Marekani kuchukua hatua madhubuti kushughulikia matatizo yake ya haki za binadamu, na kujibu matarajio ya wananchi wa Marekani na wasiwasi wa kimataifa.

Ripoti hiyo imesema kuwa hali ya haki za binadamu nchini Marekani iliendelea kuzorota mwaka 2023, na kuwa haki za binadamu zinazidi kuwa zenye mgawanyiko mkubwa nchini humo. Ripoti hiyo imesema, Wakati kundi dogo la watawala linashikilia ushawishi wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii, watu wengi wa kawaida wanazidi kutengwa, huku haki zao za msingi na uhuru vikipuuzwa.

Ikiweka wazi kuwa haki za kiraia na kisiasa zimekuwa maneno matupu nchini Marekani, ripoti hiyo inaangazia matatizo yanayoendelea kuwa mabaya zaidi, ikiwa ni pamoja na mashambulio ya risasi, mapigano ndani ya vyama, ukatili wa polisi na mfumo usiofaa wa uwajibikaji wa utekelezaji wa sheria, wingi wa wafungwa na kazi za kulazimishwa, mgawanyiko wa kisiasa, udanganyifu wa uchaguzi, na kupungua kwa uaminifu wa serikali.

Ripoti hiyo ilisema,"ugonjwa sugu wa ubaguzi wa rangi unaendelea nchini Marekani," ikisisitiza kuwa Wamarekani wenye asili ya Afrika wanakabiliwa na ubaguzi wa rangi na ukosefu wa usawa katika nyanja kama vile utekelezaji wa sheria na huduma za afya. Iliongeza kuwa Wamarekani wenye asili ya Asia wamekumbana na ubaguzi ulioongezeka, haki za Wamarekani wa asili zimekiukwa kila mara, na "itikadi ya ubaguzi wa rangi inasambaa kwa kasi nchini Marekani na kuvuka mipaka."

Ripoti hiyo ilisema ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kijamii unaendelea kufanya maisha kuwa magumu sana kwa watu maskini, na kusema Marekani imekuwa ikikataa kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kitamaduni. Ilisema haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni zinanyanyapaliwa kama "jibini ya ustawi" nchini Marekani, na hali ya "umasikini katika kazi" imeenea, huku pengo kati ya matajiri na maskini likizidi kuwa kubwa.

Ripoti hiyo ilisema Marekani haijaridhia Mkataba wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake, na inabaki kuwa mjumbe pekee wa Umoja wa Mataifa ambaye hajaridhia Mkataba wa Haki za Mtoto, ikionya kuhusu ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto unaoendelea nchini humo, huku wanasiasa “wakipuuza haki na ustawi wa wahamiaji."

Ripoti hiyo pia ilisema, nje ya nchi, Marekani kwa muda mrefu imetumia mabavu, imekuwa ikitumia siasa za upendeleo na za nguvu, na kusababisha migogoro ya kibinadamu. Nchini Marekani, haki za binadamu kimsingi ni haki inayofurahiwa na wachache tu. Matatizo mbalimbali ya haki za binadamu nchini humo yanatishia na kuzuia maendeleo mazuri ya haki za binadamu duniani.

Ripoti hiyo inajumuisha Utangulizi; Haki za Kiraia na Kisiasa Zinakuwa Maneno Matupu; Ugonjwa Sugu wa Ubaguzi wa Rangi; Kuongezeka kwa Ukosefu wa Usawa wa Kiuchumi na Kijamii; Ukiukwaji wa Haki za Wanawake na Watoto Unaendelea; Mapambano ya Kusikitisha ya Wahamiaji Wasio na Hati; na Matumizi ya Mabavu ya Marekani Yanasababisha Migogoro ya Kibinadamu.