Nchi za Afrika zahimizwa kutumia suluhu za asili ili kuharakisha maendeleo
2024-05-29 09:11:16| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Uchumi wa Afrika (UNECA) imetoa mwito kwa nchi za Afrika kutumia suluhu za asili ili kuharakisha utekelezaji wa matarajio makuu ya maendeleo.

Akihutubia kikao cha mwaka cha Muungano wa Mtaji wa Asili wa Afrika kilichofanyika huko Nairobi, nchini Kenya, naibu katibu mtendaji wa UNECA Bw. Antonio Pedro, amesema suluhu za asili zinatoa njia ya kipekee kwa Afrika kuharakisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na Ajenda ya 2063 ya Afrika, huku zikitoa mchango kwa hifadhi ya viumbe anuai vilivyosheheni katika bara hilo na kuimarisha uvumilivu wa tabianchi.

Bw. Pedro amesema, kupitia ubunifu wa makini wa njia yake ya maendeleo, Afrika inaweza kutumia thamani ya maliasili yake kupitia usimamizi wa majukumu unaotambua kikomo cha sayari, kutimiza uwiano wa ukuaji wa kiuchumi kwa uhifadhi wa mazingira na usawa wa jamii.

Kikao cha mwaka cha Muungano wa Mtaji wa Asili wa Afrika kimefanyika chini ya kaulimbiu ya “Kutumia Asili kwa Mabadiliko Endelevu ya Afrika: Kujenga Ustahimilivu katika Mazingira ya Kifedha ya Afrika”.