Xi ahimiza maendeleo ya ubora wa juu ya barabara za vijijini
2024-05-29 19:21:41| cri

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ametoa maagizo muhimu kuhusu kuendeleza ujenzi wa "Barabara Nzuri za Vijijini katika Pande Nne." Alieleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, wizara ya uchukuzi na idara husika pamoja na maeneo mbalimbali zimefuata kwa umakini maamuzi na mipango ya Kamati Kuu ya CPC kwa kuendelea na juhudi za kukabiliana na changamoto mbalimbali na ujenzi wa "Barabara Nzuri za Vijijini katika Pande Nne" umepata mafanikio makubwa, na hisia za kunufaika, kufurahia, na kuwa salama miongoni mwa watu wa vijijini zimeendelea kuimarika. Barabara za vijijini zimekuwa njia za mafanikio, furaha, kuunganisha mioyo, na kuinua uchumi wa watu wa vijijini.

Mkutano wa kitaifa wa mwaka 2024 kuhusu maendeleo ya ubora wa juu ya "Barabara Nzuri za Vijijini katika Pande Nne" ulifanyika tarehe 29 Mei huko Shaoxing, mkoani Zhejiang. Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Naibu Waziri Mkuu He Lifeng, alisoma maagizo muhimu ya rais Xi Jinping na kutoa hotuba katika mkutano huo.