Wataalamu wakutana Kenya kujadili njia za kukabiliana na dharura za ukame katika Afrika Mashariki
2024-05-29 09:18:05| CRI

Wataalamu jana walikutana huko Nairobi nchini Kenya na kujadili njia za kukabiliana na dharura za ukame katika eneo la Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na wadau 150 kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), ili kuimarisha ushirikiano katika kuboresha uwezo wa kukabiliana na maafa ya ukame katika ardhi kame na nusu kame.

Naibu katibu mtendaji wa IGAD, Mohamed Ware, alisema kuwa watu wa jamii za mpakani, wengi wao ni wafugaji na wafugaji wa kilimo, ambao wanategemea mvua zinazoendelea kutokuwa na uhakika. Kutokana na kukosekana kwa miundombinu katika maeneo ya mpakani, juhudi za kibinadamu na misaada mara nyingi zinakuwa chache na zinachelewa mno kwa wahanga.

Alitoa wito kwa eneo hilo kutekeleza mifumo thabiti ya tahadhari za mapema ili kuboresha uwezo wa kutabiri na kukabiliana na majanga ya ukame.