Bi. Peng Liyuan akutana na mke wa Rais wa Guinea ya Ikweta hapa Beijing
2024-05-29 08:57:06| CRI

Mke wa Rais wa China Bi. Peng Liyuan jana Jumanne alikunywa chai pamoja na mke wa Rais wa Guinea ya Ikweta Bi. Constancia Mangue de Obiang hapa Beijing.

Bi. Peng Liyuan amesema, China na Guinea ya Ikweta ni marafiki wakubwa na washirika wazuri wanaosaidiana, akieleza matumaini kuwa pande hizo mbili zitaimarisha mawasiliano na ushirikiano, kulinda kwa pamoja haki na maslahi ya wanawake, na kuboresha kwa pamoja kiwango cha elimu na afya ya umma kwa watu wa nchi hizo mbili.

Naye Bi. Constancia amepongeza juhudi za China, hasa alizofanya Bi. Peng Liyuan kwa ajili ya afya na maslahi ya wanawake na watoto katika nchi za Afrika, ikiwemo Guinea ya Ikweta, na anatarajia kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na China ili kuendeleza urafiki kati ya nchi hizo mbili.