Xi ahimiza kazi za usalama wa umma kuwa za kisasa
2024-05-29 19:20:50| cri

Rais Xi Jinping wa China amewataka polisi kufanya kazi za usalama wa umma kuwa za kisasa.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Jeshi, alitoa matamshi hayo Jumanne alipokutana na maafisa wa polisi waliokuwa wakihudhuria mkutano wa kitaifa kuhusu kazi za usalama wa umma mjini Beijing.