Nchi za Afrika zatakiwa kuboresha masuluhisho yanayotokana na asili ili kuongeza kasi ya maendeleo
2024-05-29 10:58:18| cri

Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imetoa wito kwa nchi za Afrika kuboresha masuluhisho ya asili ya maendeleo ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa matarajio yao ya maendeleo.

Naibu katibu mkuu wa UNECA Antonio Pedro amesema katika mkutano wa mwaka wa Muungano wa Mtaji wa Asili wa Afrika uliofanyika mjini Nairobi, Kenya, kuwa masuluhisho ya kiasili yanawakilisha njia ya kipekee ya Afrika kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Ajenda ya Afrika ya mwaka 2063, huku yakichangia katika kulinda utajiri wa anuai ya viumbe katika bara hilo na kuboresha hali ya hewa.

Amesema kwa kupanga vizuri njia zake za maendeleo, Afrika inaweza kuboresha thamani ya maliasili yake kupitia usimamizi mzuri wa uwajibikaji unaotambua mipaka ya ardhi na kuweka uwiano kati ya ukuaji wa uchumi na uhifadhi wa mazingira pamoja na haki ya jamii.