Marais wa China na UAE wafanya mazungumzo
2024-05-30 19:49:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na Rais Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambaye anafanya ziara ya kiserikali nchini China na kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu, leo katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Katika mazungumzo yao, Rais Xi amesema anaamini kuwa ziara hiyo ya Rais Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan itahimiza maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Kwa upande wake Rais Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan ameeleza kuwa, UAE ni mwenzi muhimu wa kimkakati wa pande zote wa China, na China siku zote inaweka UAE katika nafasi muhimu katika mawasiliano ya kidiplomasia kati yake na nchi za Mashariki ya Kati. Pia amesisitiza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na UAE umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo, na kutoa mfano mzuri kwa uhusiano kati ya China na nchi nyingine za kiarabu katika zama mpya.