Timu ya matibabu ya China na shirika la hisani waleta furaha kwa watoto wa Zimbabwe
2024-05-30 09:14:02| CRI

Timu ya 21 ya matibabu ya China kwa kushirikiana na shirika la hisani la Chinese Loving Mum, wameandaa shughuli maalum ya watoto mjini Harare, kabla ya ujio wa Siku ya Kimataifa ya Watoto.

shughuli hiyo iliyofanyika katika Nyumba ya Watoto ya Hossana Love in Africa iliyoko kwenye kitongoji cha kaskazini cha Harare, ilileta furaha kwa watoto wa shule ya msingi, ambao walishiriki kwenye michezo mbalimbali ikiwemo kujifunza aina moja ya mazoezi ya viungo ya kichina iitwayo “Baduanjin”.

Madaktari wa China pia walitumia fursa hii kuonesha mbinu za huduma ya kwanza kwa watoto, ambao waliitikia kwa shauku.

Kiongozi wa timu ya madaktari ya China, Tan Jianlong amesema, shughuli hiyo inalenga kutoa huduma za afya kwa wenyeji na kuboresha uwezo wa wafanyakazi wa afya wa huko wa kutambua na kutibu magonjwa mbalimbali.