Kulingana na ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD), takriban watu milioni 74.9 katika eneo la Pembe ya Afrika wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.
Ripoti hiyo ilisema kati ya idadi hiyo, watu milioni 46.8 wanatoka nchi saba kati ya wanachama wanane wa IGAD zikiwemo Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania, Sudan na Uganda, na nyingine ni Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Ripoti hiyo ilisema kuwa kupanda kwa idadi ya watu wenye uhaba wa chakula katika eneo hilo kutoka watu milioni 58.1 mwezi Februari hadi sasa kumetokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.