Takwimu kutoka Kituo cha Utafiti wa Afya katika Chuo Kikuu cha Rutgers cha Marekani zimeonesha kuwa, karibu asilimia 60 ya Wamarekani wenye asili ya Afrika wanakabiliwa na aina mbalimbali za vurugu za matumizi ya bunduki, na waathirika wengi wanaishi katika jamii yenye mapato ya chini. Watafiti wameeleza kuwa, matokeo hayo yamethibitisha kuwa, Wamarekani hao wenye asili ya Afrika wanaendelea kuathiriwa vibaya kutokana na hali hiyo.
Ukweli ni kwamba, hii ni sehemu ndogo tu ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Marekani. Ripoti ya mwaka 2023 kuhusu Ukiukwaji wa Haki za Binadamu nchini Marekani iliyotolewa tarehe 29 mwezi huu na serikali ya China imefafanua kwa dunia nzima ukweli kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Marekani, ikitumia asilimia kubwa ya data na kesi zikiwa ni pamoja na hali ya ubaguzi wa rangi, kuongezeka kwa pengo kati ya matajiri na maskini, mapambano makali kati ya vyama, na ubaguzi dhidi ya wahamiaji. Kutokana na hayo, watu wametambua wazi kuwa, kile kinachoitwa “haki za binadamu za mtindo wa Marekani” ni za watu wachache tu, na pia zinaonesha umwamba wa Marekani. Kutokana na machafuko yake yenyewe, ni kitendo cha kikejeli kwa baadhi ya wanasiasa wa Marekani kujisifu kwa kutumia “Haki za Binadamu”, na wale wanaojidai kama “majaji wa haki za binadamu” wanatakiwa kuhukumiwa zaidi.