Msomi wa Afrika: Ziara ya Rais Xi Jinping yatia uhai mpya katika ushirikiano kati ya China na Ulaya
2024-05-30 14:28:03| CRI

Habari za wakati huu msikilizaji na karibu tena kwenye kipindi cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CGTN Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo, licha ya habari mbalimbali kuhusu pande hizo mbili, pia tutakuwa na ripoti inayohusu msomi wa Afrika anayezungumzia ziara ya Rais wa China Xi Jinping katika nchi za Ulaya, kwamba inaleta uhai mpya katika ushirikiano kati ya China na Ulaya, pia tutakuwa na mahojiano kutoka CGTN Idhaa ya Kiswahili Nairobi yatakayozungumzia Shindano la 23 la "Daraja la Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambalo limefanyika hivi karibuni nchini Kenya.