Serikali ya Tanzania yatenga Sh Bil. 61.5 kwa ujenzi wa barabara za mikoa
2024-05-30 23:06:59| cri

Serikali ya Tanzania imesema kiasi cha Sh Bil.61.5 kimetengwa kwa ajili ya barabara na madaraja katika mikoa yote 26 Tanzania Bara katika mwaka wa fedha 2024/25.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 bungeni mjini Dodoma hapo jana, Waziri wa Ujenzi nchini Tanzania, Innocent Bashungwa amesema kazi zilizopangwa ni ukarabati wa kilomita 600 za barabara kwa kiwango cha changarawe, kujenga kilometa 60 barabara kwa kiwango cha lami, na ujenzi wa madaraja na makalavati 70.

Aidha, amesema kati ya fedha hizo, Sh milioni 726.00 zitatumika kwa ajili ya programu ya mafunzo kwa vitendo kwa wahandisi wahitimu.