IMF laongeza makadirio ya ukuaji wa pato la taifa la China mwaka 2024 hadi asilimia 5
2024-05-30 09:38:56| CRI

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeongeza makadirio ya ukuaji wa pato la taifa (GDP) la China mwaka 2024 kutoka asilimia 4.6 ya Aprili hadi asilimia 5.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF Bi. Gita Gopinath amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari baada ya timu ya shirika hilo kutembelea China kuanzia tarehe 16 hadi 28 mwezi huu. Ameeleza kuwa marekebisho hayo ya makadirio yamehimizwa na ukuaji wenye nguvu wa pato la taifa la China katika robo ya kwanza ya mwaka huu pamoja na sera mbalimbali zilizotolewa hivi karibuni.

Amesema China inafanya kazi muhimu na ya kiujenzi katika kusaidia urekebishaji wa madeni katika nchi dhaifu na zenye pato la chini na kuhimiza mpito kwa uchumi wa kijani. IMF inatarajia kuendelea kushirikiana na China kwenye suala hili.