Hatua ya Ujenzi wa Jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja kuharakishwa
2024-05-31 14:08:21| cri

Rais wa China Xi Jinping amesema jana kuwa, nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Pili wa Kilele wa China na Nchi za Kiarabu wa mwaka 2026, akiamini kuwa huu utakuwa mnara mwingine katika uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu.

Rais Xi amesema hayo jana wakati alipohutubia Ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu. Hayo ni matokeo muhimu zaidi ya mkutano huo.

Rais Xi pia ametoa mpango kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili katika kipindi kijacho, na wazo kuhusu “Kujenga Mifumo Mitano Mikbuwa ya Ushirikiano”, ili kuharakisha ujenzi wa Jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye Mustakabali wa Pamoja.

Huu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu. Katika miaka 20 iliyopita, uhusiano kati ya pande hizo mbili umeshinda changamoto mbalimbali za kimataifa, na kutoa mfano mzuri wa kuigwa kwa ushirikiano wa Kusini-Kusini. Ushirikiano kati ya pande hizo mbili umezidi kuimarishwa, haswa tangu Mkutano wa Kwanza wa China na Nchi za Kiarabu ulipoweka mpango wa “Kujenga kwa nguvu zote Jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye Mustakabali wa Pamoja katika Zama Mpya”. Hadi sasa Pendekezo la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, limetekelezwa katika nchi zote za Kiarabu, na kuwanufaisha watu karibu bilioni 2 wa pande hizo mbili. “Hatua Nane Kuu za Pamoja” za ushirikiano wa kiutendaji kati ya China na nchi za kiarabu zimepata mafanikio makubwa katika hatua ya mwanzo.

Hivi sasa dunia imeingia katika kipindi chenye misukosuko na mabadiliko. China na nchi za Kiarabu ambazo zinakabiliwa na majukumu ya kustawisha taifa na kuharakisha ujenzi wa nchi, zina hamu kubwa ya kuimarisha ushirikiano. Tokea mwaka uliopita, maafikiano ya kihistoria kati ya Saudi Arabia na Iran, na mazungumzo kati ya Hamas na Fatah yaliyofanyika mjini Beijing, zimezifanya nchi za Kiarabu kutambua kuwa, China imekuwa ikisaidia kwa moyo wa dhati eneo la Mashariki ya Kati kutafuta amani na maendeleo. Kutokana na hayo, mkutano huo unaoendelea mjini Beijing ambao ni wa kwanza wa mawaziri wa China na nchi za Kiarabu baada ya Mkutano wa kwanza wa kilele kati ya pande hizo mbili, una umuhimu mkubwa sana.

China na nchi za Kiarabu zitachukua mkutano huo kuwa mwanzo mpya, kuimarisha ushirikiano utakaoleta matokeo makubwa zaidi katika miaka 20 ijayo, na kuingiza utulivu na uhakika kwa dunia yenye misukosuko.