Waziri wa Mambo ya Nje wa China atoa wito kwa China na Russia kuleta manufaa zaidi kwa watu wao
2024-05-31 14:03:03| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema China itashirikiana na Russia katika kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa usalama na utulivu wa dunia kupitia uratibu wa kimkakati wa ngazi ya juu.

Wang amesema hayo kwa njia ya video kwenye kongamano la ngazi ya juu la washauri mabingwa kutoka nchi hizo mbili. Amesema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Russia miaka 75 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepitia majaribu mengi na kuwa imara na kuweza kuhimili changamoto zaidi, na kujenga mfano wa uhusiano wa kimataifa na uhusiano kati ya nchi jirani kubwa.