Benki ya Maendeleo ya Afrika yazindua mpango mkakati wa kuhimiza ukuaji jumuishi barani Afrika
2024-05-31 08:53:19| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imezindua mpango mkakati wa miaka kumi ambao umeeleza jinsi benki hiyo itakavyosaidia bara la Afrika kuhimiza ukuaji jumuishi wa kijani na uchumi imara.

Rais wa AfDB Akinwumi Adesina aliwaambia waandishi wa habari huko Nairobi, Kenya kwamba mkakati huo pia unaeleza jinsi benki hiyo itakavyowekeza katika rasilimali bora barani Afrika, ambayo ni idadi ya vijana inayotoa fursa isiyo na kifani ya kidemografia katika kanda hiyo. Licha ya hayo, mpango huo pia unazingatia usimamizi wa kiuchumi na kutambua umuhimu wa kimkakati wa wanawake katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi barani Afrika.

Kwa mujibu wa Bw. Adesina, mpango huo umejikita katika dira ya Afrika kama inavyoonyeshwa katika Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika, ambayo inalenga kuleta mabadiliko kwa watu wa Afrika.