Milipuko ya magonjwa yaongezeka katika pembe ya Afrika baada ya mvua kubwa kunyesha
2024-05-31 09:00:43| CRI

Ripoti kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD) jana ilisema kuwa eneo la pembe ya Afrika limerekodi ongezeko la milipuko ya magonjwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha mafuriko makubwa.

Kulingana na ripoti hiyo, magonjwa ambayo yamerekodiwa ni pamoja na kipindupindu, malaria, surua, homa ya kidingapopo, homa ya manjano, polio na kimeta, ambayo yote yanahusisha moja kwa moja na hali mbaya ya hewa.

IGAD ilisema kuwa Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan na Uganda zinashughulikia milipuko ya kipindupindu, iliyosababishwa na mafuriko ya hivi karibuni. Nchini Ethiopia, kesi 14,632 na vifo 114 viliripotiwa kutoka maeneo 90 katika mikoa 11 kati ya tarehe 1 mwezi Januari hadi tarehe 28 mwezi Aprili.