China na nchi za kiarabu zafikia Taarifa ya Pamoja kuhusu suala la Palestina
2024-05-31 14:05:59| cri

Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu ulifanyika Beijing tarehe 30, Mei, ambapo pande hizo mbili zilijadiliana kwa kina suala la Palestina, na kufikia taarifa ya pamoja kuhusu suala hilo.

Pande hizo mbili zinaona kwamba maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, likiwemo azimio nambari 2728 la Baraza la Usalama, ni lazima yatekelezwe kikamilifu na kwa ufanisi, na zitafanya juhudi za pamoja ili mapigano katika Ukanda wa Gaza yasimamishwe, na suala la Palestina lipate suluhu kamili, lenye haki na la kudumu mapema iwezekanavyo