Safari ya meli kutoka Weihai, China kwenda Zanzibar, Tanzania yazinduliwa rasmi
2024-05-31 08:44:10| CRI

Safari ya meli kutoka mji wa Weihai, China kwenda visiwani Zanzibar, Tanzania ilizinduliwa rasmi jana Mei 29. Hii ni njia ya kwanza ya meli inayokwenda Afrika kufunguliwa kutoka bandari ya Weihai, na pia ni njia ya kwanza ya moja kwa moja ya baharini kutoka China kwenda bandari ya Zanzibar.

Saa nne asubuhi, meli ya Tina iliyobeba tani 830 za mizigo ikiwemo magari ya uhandisi na mabomba ya metali iliondoka polepole kwenye bandari ya Weihai mkoani Shandong, ikiashiria kufunguliwa rasmi kwa njia ya bahari ya kutoka forodha ya Weihai kwenda bara la Afrika. Meli hiyo inatarajiwa kuwasili bandari ya Zanzibar baada ya safari ya siku 30. Meneja mkuu wa kampuni ya mnyororo wa ugavi ya Huatan ya mji wa Weihai Bw. Liu Youzhi amesema kwa furaha kuwa, baada ya kuzinduliwa kwa safari hii, muda wa kusafirisha bidhaa zao kwenda Afrika utapungua kutoka siku zaidi ya 70 hadi kufikia siku 30 hivi, na gharama pia itapungua kwa nusu.

“Zamani mizigo ilifika bandari ya Weihai baada ya kuzunguka kupitia bandari ya Tianjin au bandari ya Shanghai, baada ya kufunguliwa kwa njia hii inayokwenda moja kwa moja nchini Tanzania, gharama za uchukuzi pia zitapungua kwa nusu.”

Baada ya njia ya baharini kutoka Weihai kwenda Zanzibar kuzinduliwa, itatoa huduma za uchukuzi hasa kwa makampuni ya China yanayofanya biashara barani Afrika kusafirisha mashine za uhandisi na vifaa vya ujenzi, ili kuhimiza bidhaa za viwandani kuuzwa Afrika. Forodha ya Weihai imechukua hatua mbalimbali za kurahisisha taratibu za kukagua na kupitisha mizigo, ili kuhakikisha meli na bidhaa zinapita kwenye forodha kwa ufanisi na kwa urahisi. Naibu maneja mkuu wa bandari ya Weihai Bw. Fang Yong anasema:

“Tumetumia mbinu maalumu ya huduma za maghala, na kutoa huduma za kituo-kimoja kwa makampuni kuweka oda, kuhifadhi bidhaa, kukagua mizigo, kupata kibali, na kupakia na kupakua mizigo.”

Huu ni mwaka wa 60 tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi, ikiwa ni matunda mapya ya ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya nchi hizo mbili, uzinduzi wa njia ya baharini ya kutoka Weihai kwenda Zanzibar, utaweka daraja jipya kwa ajili ya kuhimiza muunganiko wa miundombinu, ufanisi wa biashara na maingiliano ya watu wa pande hizo mbili. Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Khamisi Mussa Omar anasema,

“Ushirikiano kati ya China na Afrika una mustakbali mkubwa, tunapaswa kufanya juhudi kwa pamoja kuhakikisha pande zote mbili za njia hii zina bandari na miundombinu ya kiwango cha juu cha kimataifa, ili kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo, na kuiwezesha njia hii ya baharini kuleta manufaa makubwa zaidi ya kiuchumi.”

 

 

“威海-坦桑尼亚”航线正式开通

 

昨天(0529),“威海-坦桑尼亚”航线正式开通,这是威海口岸开通的首条对非国际航线,也是中国到非洲坦桑尼亚桑给巴尔港的首条直达航线。

点音频:威海-坦桑航线

 

【压混……】

上午十点,随着搭载着工程车辆、金属管件等830吨货物的“蒂娜”轮缓缓驶离山东港口威海港,威海口岸首条对非航线正式开通。预计30天后,“蒂娜”轮将抵达坦桑尼亚桑给巴尔港。从事中非贸易多年的威海华坦供应链管理有限公司总经理刘有志高兴地表示,航线开通后,他们发往非洲的货物,运输时间将从70多天压缩到30天左右,节省一半的物流成本。

【以前都是从天津港或者是上海港这样的航运线中转来到威海港,这条航线开通以后,直达坦桑尼亚,(现在物流)资金成本也能节省一半。】

“威海-坦桑尼亚”航线开通后,将重点为在非中资企业提供工程机械、建筑材料等运输服务,助力中国工业制品出口非洲。为保障这条中非物流大通道顺畅、高效、安全运行,威海口岸采取“预约通关+优先查验”等措施,确保船舶快速检疫、货物高效通关。山东港口威海港党委委员、副总经理、安全总监 方勇:

【我们采用了中非集分仓服务模式,为广大企业提供订仓、仓储、查验、放行、装卸等一站式全链条服务。】

今年是中坦建交60周年,作为中坦共建“一带一路”的最新成果,“威海-坦桑尼亚”航线的开通,将为促进中非设施联通、贸易通畅、民心相通架起新桥梁。坦桑尼亚驻华大使哈米斯·穆萨·奥马尔:

【中非合作前景广阔,我们需要共同努力,确保航线两端都拥有世界一流的港口和基础设施配套,提升货物贸易装载量,使航线带来更多的经济福祉。】