Rais Xi Jinping wa China leo tarehe 31, Mei alifanya mazungumzo na mwenzake wa Tunisia Kais Saied, ambaye alikuja China kwa ziara ya kiserikali na kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu.
Rais Xi Jinping amesema mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tunisia. Katika miaka hii 60, haijalishi jinsi hali ya kimataifa inavyobadilika, China na Tunisia zimekuwa zikiheshimiana, kutendeana kwa usawa, na kuungana mikono, zikiandika ukurasa mpya wa nchi zinazoendelea kusimama pamoja na kusaidiana mbele ya changamoto mbalimbali. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Tunisia kudumisha urafiki wa jadi, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie kwenye ngazi mpya.