Maabara ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) nchini Tanzania imepata ithibati ya kimataifa ya kutambulika kama maabara bora duniani.
Ithibati hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) kama maabara inayoaminika katika vipimo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa JKCI Dk Peter Kisenge amesema hatua hiyo kubwa imetokana na kwamba vipimo vya maabara hiyo kwa sasa vinaaminika kitaifa. Amesema kutokana na kupata ithibati nchi yoyote inaweza kuleta vipimo na vikafanyika hapo hususani wale wanaofanya tafiti hata za kidunia.
Aidha amefafanua kuwa maabara hiyo ina uwezo wa kupima magonjwa mengine ya kuambukiza na yasiyoambukiza huku wakitarajia kupata maabara kubwa zaidi.