Kenya imezindua mpango mkakati unaolenga kuongeza biashara ya nje ya nchi hiyo kwa asilimia 10 kwa mwaka kutoka shilingi trilioni moja za Kenya zilizorekodiwa mwaka jana.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kutangaza Biashara ya Nje na Chapa ya nchini Kenya Jaswinder Bedi amewaambia wanahabari jijini Nairobi kwamba, mpango mkakati huo unatumika kama ramani ya kuifanya Kenya kuwa nchi ya uchumi unaoongozwa na biashara ya nje na chapa kubwa duniani.
Ameongeza kuwa, mpango mkakati huo unatoa utaratibu utakaowezesha Kenya kupanua biashara yake ndani ya bara la Afrika, ambalo ni soko kubwa la nchi hiyo, kwa kuongoza katika utekelezaji kamili wa Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA).