Rais wa Kenya atangaza mikakati ya kuondokana na njaa nchini humo
2024-06-03 22:25:29| cri

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake imeandaa mikakati ya kupunguza njaa na umasikini nchini humo kupitia kilimo na kuimarisha uchumi.

Akihutubia wananchi katika Maadhimisho ya 61 ya Madaraka Dei Jumamosi iliyopita, rais Ruto amesisitiza umuhimu wa kilimo kwa uchumi wa nchi hiyo, akisema serikali yake haitaacha nyuma sehemu ya jamii au eneo lolote katika kukabiliana na uhaba wa chakula na umasikini.

Rais Ruto amesema serikali yake imeshirikiana na wakulima na wadau wengine katika mfumo wa thamani wa kilimo, wakiwemo wasambazaji na watengenzaji pembejeo kubadilisha kilimo cha wakulima wa mashamba madogo ili kutimiza utoshelevu wa chakula nchini humo.