Sudan na Sudan Kusini zajadili kurejesha usafirishaji wa mafuta
2024-06-03 09:07:36| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala wa Sudan Abdel Fattah Al-Burhan Jumapili alifanya mazungumzo na Mshauri wa Rais wa Mambo ya Usalama wa Taifa wa Sudan Kusini Tut Gatluak juu ya kurejesha usafirishaji wa mafuta wa Sudan Kusini kupitia ardhi ya Sudan.

Taarifa iliyotolewa na baraza hilo la utawala ilimnukuu Gatluak akisema kuwa njia ya usafirishaji wa mafuta ya Sudan Kusini imeathiriwa na vita nchini Sudan, na kwa sasa imesitishwa kutokana na opresheni za kijeshi zinazoendelea kwenye maeneo yaliyoko kwenye njia hiyo. Amesema wizara za mafuta za nchi mbili zimekubali kufanya mkutano kwa ajili ya kujadili ufumbuzi wa kutatua suala hilo.

Taarifa hiyo ilisema Gatluak pia aliwasilisha ujumbe wa maandishi kutoka kwa rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan Kusini juu ya maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.