OPEC+ yaendelea kupunguza uzalishaji wa mafuta
2024-06-03 08:55:56| CRI

Shirika la Nchi Zinazouza Petroli (OPEC) na washirika wake, kundi linalojulikana kama OPEC+, wameamua kudumisha kwa kiasi kikubwa viwango vya uzalishaji kwa wanachama wake hadi mwaka 2025, na kuendelea kupunguza uzalishaji wa mafuta.

Kufuatia mkutano wa kawaida wa mawaziri wa mafuta wa OPEC+, OPEC imetoa taarifa kwamba kiwango cha jumla cha uzalishaji wa mafuta ghafi kwa nchi za OPEC+ kitaendelea hadi mwaka mzima wa 2025.

Kiwango cha uzalishaji kwa nchi za OPEC+ mwaka ujao kitasalia sawa na mwaka huu isipokuwa kwa Umoja wa Falme za Kiarabu. Uzalishaji wa UAE utapanda na kufikia hadi mapipa milioni 3.519 kwa siku, huku ongezeko hilo likianza polepole kuanzia Januari 2025 hadi mwishoni mwa Septemba 2025.

Zoezi la kupunguza uzalishaji wa OPEC+ litaendelea hadi robo ya tatu ya mwaka huu.