Watu 12 wafariki kutokana na mafuriko nchini Afrika Kusini
2024-06-04 10:44:42| cri

Watu 12 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika pwani ya Afrika Kusini.

Msemaji wa manispaa ya Ghuba ya Nelson Mandela katika Mkoa wa Cape Mashariki amesema, idadi ya watu waliofariki mpaka sasa kutokana na mafuriko hayo ni 7.

Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na serikali ya Mkoa wa Kwa-Zulu Natal nchini humo imesema, watu watano wamefariki katika mji wa eThekwini, ambao umeathirika zaidi na mafuriko hayo, huku watu wengine kadhaa wakiendelea kupata matibabu kutokana na majeraha waliyopata.