Wizara ya Afya ya Sudan Jumatatu ilisema kuwa jumla ya tani 20 za dawa za kuokoa maisha zilidondoshwa kwa helikopta huko El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, kufuatia kuongezeka kwa mapambano kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
Waziri wa Afya Haitham Mohamed Ibrahim alitoa taarifa akisema vitu hivi vilisafirishwa ikiwa ni miongoni mwa juhudi zake za kutoa huduma za kimsingi za afya nchini kote. Aliongeza kuwa dawa na vifaa vingine vya matibabu tani 30 vimepangwa kusafirishwa katika jimbo la Darfur Kaskazini.
Wakati huohuo, mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Kitaifa wa Vifaa vya Matibabu nchini Sudan amethibitisha kwenye taarifa akisema, kitendo hicho cha kudondosha misaada huko El Fasher kimefanikiwa bila ya kuwa na hasara yoyote kubwa.