AU yaonya juu ya kuongezeka kwa machafuko na mabadiliko ya serikali yasiyofuata katiba barani Afrika
2024-06-05 22:47:37| cri

Umoja wa Afrika (AU) umetoa onyo kuhusu athari za pamoja za kuongezeka kwa mapigano na mabadiliko ya serikali yasiyofuata katiba ambayo yanatishia misingi ya demokrasia na usalama wa nchi za Afrika.

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa Idara ya Kudhibiti Mapigano iliyo chini ya Idara ya Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama ya Kamati Kuu ya Umoja wa Afrika, Alhaj Sarjoh Bah alipohutubia mkutano wa amani na usalama wa Afrika uliofanyika jumatatu katika makao makuu ya Umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Ametoa wito kwa juhudi za pamoja katika kuimarisha zaidi amani na usalama barani humo, ikiwa ni pamoja na uwepo wa Kikosi cha Dharura za Afrika chenye uwezo wa kukabiliana na mapigano na matukio ya dharura katika bara hilo.