Pembe ya Afrika kukabiliwa na duru mpya ya mvua kubwa
2024-06-05 08:54:12| CRI

Kituo cha Utabiri na Usimamizi wa Hali ya Hewa (ICPAC) cha Shirika la Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) Jumanne kilisema, nchi kadhaa za Pembe ya Afrika zitakabiliwa na duru mpya ya mvua kubwa itakayosababisha mafuriko.

ICPAC ilithibitisha kwenye utabiri mpya ikisema Sudan Kusini, Ethiopia na Kenya zitakabiliwa na mvua kubwa kati ya milimita 50 na milimita 200. Inakadiriwa kuwa mvua kubwa isiyo ya kawaida itanyesha kwenye sehemu nyingi za kusini mwa Sudan, kaskazini na mashariki mwa Sudan Kusini, magharibi mwa Ethiopia, kaskazini mwa Uganda na magharibi mwa Kenya.

ICPAC pia inakadiria kuwa joto litapanda zaidi ya kawaida kwenye sehemu nyingi za Pembe ya Afrika.