Serikali ya Sudan yaomba msaada zaidi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa
2024-06-05 08:51:56| CRI

Serikali ya Sudan kupitia Wizara yake ya Mambo ya Nje, Jumanne ilitoa taarifa ikiitaka jumuiya ya kimataifa kutoa msaada zaidi kwa wale walioathiriwa na mzozo wa kijeshi unaoendelea nchini humo, hasa wa dawa, suluhu za uingiliaji kati, na matibabu.

Tangu Mei 10, mapigano makali yamezuka El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, na maeneo yanayozunguka kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF), ambayo yanazuia kupita kwa misafara ya misaada kwenye Kivuko cha Al-Tina na Chad.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limeonya kuwa vita vinavyoendelea nchini Sudan vinahatarisha kuzusha janga kubwa zaidi la njaa duniani katika nchi ambayo inashuhudia msukosuko mkubwa zaidi wa watu kukimbia makazi yao. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, nusu ya wakazi wa Sudan, ambao ni watu milioni 25 wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi, huku karibu watu milioni 18 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.