Kenya yaandaa maonyesho ya maua ikiitikia wito wa uzalishaji endelevu
2024-06-05 08:53:25| CRI

Maonesho ya 11 ya Biashara ya Kilimo cha Maua ya Kimataifa yamefunguliwa Jumanne mjini Nairobi, nchini Kenya, yakiitikia wito wa uzalishaji endelevu kama vile udhibiti jumuishi wa wadudu. Maonyesho hayo ya siku tatu yanawaleta pamoja maafisa wakuu wa serikali, wakulima wa maua na wanunuzi kutoka nchi 75 ili kukuza vitendo rafiki kwa mazingira.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, katibu mkuu ambaye pia ni afisa mhasibu wa Idara ya Taifa ya Masuala ya Baraza la Mawaziri Idris Salim Dokota amesema kauli mbiu ya maonyesho ya mwaka huu ni Uendelevu, ambayo inagusa sana dhamira ya serikali ya kukuza kilimo cha maua nchini Kenya.

Afisa mkuu mtendaji wa HPP ambaye pia ni mratibu wa maonyesho hayo Dick van Raamsdonk amesema kuwa mashamba ya maua yanaelekea katika kufuata vitendo endelevu na kupunguza kiwango chao cha kaboni ambayo yatawezesha kuuzwa kimataifa.