WB yaipongeza Tanzania kwa kasi usambazaji umeme kwa wananchi
2024-06-05 09:48:42| cri

Benki ya Dunia (WB) imeipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa kusambaza umeme kwa wananchi wake.

Akitoa pongezi hizo jana jijini Dodoma, mji mkuu wa Tanzania, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini humo, Nathan Belete amesema Benki hiyo inapanga kufanya mazungumzo zaidi na mamlaka husika na kuona namna bora zaidi ya kusaidia katika masuala ya nishati safi ya kupikia kwa kufadhili na kuhusisha sekta binafsi kwa kuangalia fursa zilizopo.

Akizungumzia pongezi hizo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Doto Biteko ameishukuru Benki ya Dunia kwa pongezi hizo na kusema Benki hiyo ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na kuwa wamekuwa na ajenda ya kushirikiana katika miradi ya nishati.