Fainali ya mashindano ya 17 ya umahiri wa lugha ya Kichina “Daraja la Kichina” kwa wanafunzi wa sekondari wa Kenya ilifanyika Jumatano katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, ambapo wanafunzi 16 walishiriki kwenye mashindano hayo.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Kenya na Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, yanaonyesha umahiri wa washiriki wa kuongea lugha ya Kichina pamoja na muziki wa jadi, dansi, Kung Fu na sanaa ya maandiko ya Kichina.
Kaimu makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Kenyatta Waceke Wanjohi amesema mashindano hayo ambayo yameshirikisha wanafunzi wa sekondari nchini kote, yanathibitisha nguvu ya ushirikiano wa kiutamaduni kati ya Kenya na China.
Mwambata anayeshughulikia masuala ya utamaduni katika ubalozi wa China nchini Kenya Tang Jianjun amesema kujifunza lugha ya Kichina kunafanya kazi muhimu katika kujenga zaidi jumuiya ya China na Kenya yenye mustakabali wa pamoja.