Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa watoa wito wa juhudi zaidi kukabiliana na uhaba wa maji na mabadiliko ya tabianchi katika Pembe ya Afrika
2024-06-06 22:58:17| cri

Benki ya Dunia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda kwa pamoja yametoa wito wa uwekezaji zaidi katika usimamizi wa maji wakati mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi ukiongeza uhaba wa maji katika Pembe ya Afrika.

Wawakilishi kutoka mashirika manane ya Umoja wa mataifa, Benki ya Dunia, Mamlaka ya Maingiliano ya Kiserikali kuhusu Maendeleo, wenzi wa kibinadamu na wa maendeleo, mashirika ya kijamii na sekta binafsi walikutana jijini Nairobi, Kenya jumanne wiki hii katika majadiliano ya kimkakati yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda kuhusu usimamizi wa maji.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, mtu mmoja kati ya watu watano katika Pembe ya Afrika anakosa maji safi na salama katika eneo hilo lililoathiriwa sana na ukame na mafuriko.