Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Chen Mingjian amesema kuwa Mazungumzo ya vijana wa China na Tanzania ni muhimu katika kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Amesema hayo katika Mazungumzo ya Vijana wa China na Tanzania yaliyofanyika Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ameongeza kuwa vijana ndio chanzo cha uhai wa kuendeleza urafiki wa dhati kati ya China na Tanzania. Mazungumzo hayo yalikuwa ni miongoni mwa shughuli mfululizo za kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Patrobas Katambi ameishukuru China kwa juhudi zake za kukuza maendeleo ya vijana. Ameongeza kuwa juhudi hizo zitasaidia kuweka mazingira mazuri ya kukabiliana na ukosefu wa ajira na matatizo ya kiakili hasa kwa vijana.