Watu 14 wafariki na wengine 14 kujeruhiwa vibaya baada ya lori kugonga magari mengi kusini mwa Tanzania
2024-06-06 08:56:44| CRI

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa vibaya Jumatano baada ya lori kugonga magari mengi, likiwemo Costa, katika mkoa wa Mbeya, Tanzania

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera, ajali hiyo ilitokea katika eneo la mlima Mbembela kwenye mteremko mkali majira ya saa 7:20 mchana kwa saa za huko, ambapo inadaiwa dereva wa lori hilo alishindwa kulimudu lori lake na kwenda kuparamia Costa, gari aina ya Harrier, bajaji na guta.

Homera alifafanua kuwa wahanga wote walikuwa abiria katika basi dogo na kwamba majeruhi, wengi wao wakiwa mahututi, walikimbizwa katika hospitali ya Mbeya. Miongoni mwa waliofariki ni wanaume wanane, akiwemo mvulana wa miaka minne.

Alisema lori hilo lililokuwa limebeba kokoto lilikuwa likitoka Dar es Salaam, na kuelekea Mbeya mjini, na basi dogo lilikuwa likitokea Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia kuelekea Mbeya.