Kenya yazindua mfumo wa ukuaji endelevu wa idadi ya watu
2024-06-07 08:52:15| CRI

Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango ya Uchumi wa Kenya Njuguna Ndung'u amesema kuwa Kenya imezindua mfumo utakaoongoza utekelezaji wa programu za idadi ya watu kwa maendeleo endelevu ya nchi.

Amesema kwamba sera hiyo itatoa mwelekeo wa haraka na uliooanishwa wa kushughulikia ongezeko la watu kuhusiana na ukuaji wa uchumi.

Anaona kuwa mfumo huo unaoitwa "Sera ya Idadi ya Watu ya Kitaifa ya Kenya kwa Maendeleo Endelevu" utaiongoza nchi hiyo kukabiliana na ongezeko la watu kulingana na Dira yake ya kiuchumi ya 2030, Ajenda ya Afrika 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.