NATO haina mpango wa kupeleka wanajeshi Ukraine
2024-06-07 08:51:26| CRI

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema Jumuiya hiyo haina mpango wa kupeleka vikosi nchini Ukraine.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na rais wa Finland Alexander Stubb katika siku ya pili ya ziara yake nchini humo, Stoltenberg alisema kuwa wanaangalia jinsi wanavyoweza kuanzisha mfumo thabiti zaidi wa msaada wao kwa Ukraine.

Akitilia mkazo msimamo wa Stoltenberg, rais Stubb pia alisema kuwa Finland haina mpango wa kutuma wanajeshi Ukraine, na kuongeza kuwa nchi hiyo iko kwenye majadiliano na washirika kuhusu njia za kuiunga mkono Ukraine.

Stoltenberg pia alibainisha kuwa hakuona tishio lolote la kijeshi kutoka Russia dhidi ya mshirika yeyote wa NATO, na hata baada ya kumalizika kwa mzozo. Alisema wazo ambalo vita nyingine inakuja hivi karibuni sio sahihi.

Rais Stubb pia ameongeza kuwa haamini kama Russia itafanya shambulizi.