Watu 16 wauawa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi la ADF nchini DRC
2024-06-07 22:59:09| cri

Watu 16 wameuawa katika mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi la ADF.

Ofisa kutoka mkoa huo ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema, watu hao waliuawa kwa kukatwa na mapanga wakiwa nyumbani kwao na mashambani, na kwamba wengine waliuawa wakati wakikimbia machafuko hayo.

Kundi la waasi la ADF limekuwa likifanya operesheni zake kutokea misitu iliyoko mashariki mwa DRC kwa miongo mitatu sasa, na mwaka 2019, kundi hilo lilijihusisha rasmi na kundi la IS.