Katibu mkuu wa UM ataka mapigano yasitishwe mpakani mwa Lebanon na Israel
2024-06-07 10:00:58| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa taarifa akitaka mapigano yasitishwe mara moja mpakani mwa Lebanon na Israel.

Kwenye taarifa hiyo, Bw. Guterres ameeleza wasiwasi wake kwamba mapigano hayo siyo tu yameharibu makazi yaliyoko karibu na mpaka wa muda wa “Mstari wa Bluu”, bali pia yameleta athari za kina kwa maeneo ya nchi hizo mbili na kuongeza mgogoro unaoweza kusababisha uharibifu mkubwa zaidi.

Pia amehimiza pande zote husika kutekeleza kikamilifu Azimio namba 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusitisha vitendo vyote vya uhasama.