Zaidi ya watu 100 wameuawa katika shambulio lililofanywa na kikosi cha RSF katika kijiji cha Wad Al-Noura, mkoa wa Gezira nchini Sudan.
Jeshi la Sudan halijatoa tamko lolote kuhusu shambulio hilo, lakini kikosi cha RSF kimesema katika taarifa yake kuwa, wapiganaji wake walishambulia kundi la Mustanfareen, ambalo linashirikiana na Jeshi la Sudan katika eneo hilo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana, Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan limekituhumu kikosi cha RSF kwa mauaji ya kimbari katika kijiji cha Wad Al-Noura, na kusema mauaji hayo yanahusika na tabia ya kushambulia raia, kupora mali zao, na kuwalazimisha kukimbia makazi yao.
Sudan imeshuhudia mapigano makali kati ya Jeshi la nchi hiyo na Kikosi cha RSF yaliyoanza April 15 mwaka jana.