Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Alhamisi lilimchagua waziri mkuu wa zamani wa Cameroon Philemon Yang kuwa mwenyekiti wa Kikao cha 79 cha UNGA.
Yang atampokea mwenyekiti wa Kikao cha 78 cha UNGA Denis Francis kutoka Trinidad na Tobago, wakati mkutano wa 79 wa UNGA utakapofunguliwa tarehe 10 Septemba huko New York.
Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, Yang amesema mbali na tofauti zao, wanapaswa kushirikiana katika kuhimiza amani, kuhakikisha kwamba hakuna vita, na kuzuia maafa kwa moyo wa umoja.
Ameongeza kuwa inatakiwa kuchukuliwa hatua kwa ajili ya kutimiza maendeleo endelevu, ustawi wa pamoja, na kuishi kwa maelewano na mazingira ya asili, ili kuhakikisha kizazi cha sasa na kijacho kinaendelea kunufaika. Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha utaratibu wa pande nyingi akisisitiza kuwa ni msingi wa kanuni na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.