Waziri mkuu wa zamani wa Cameroon achaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la UM
2024-06-07 10:01:32| cri

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana tarehe 6 limemchagua waziri mkuu wa zamani wa Cameroon Philemon Yang kuwa mwenyekiti wa Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja huo, ambaye ataingia madarakani mwezi Septemba mwaka huu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Siku hiyohiyo, nchi wanachama wa Baraza kuu hilo wamepiga kura katika Makao Makuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York na kuzichagua Denmark, Ugiriki, Pakistan, Panama, na Somalia kuwa nchi wajumbe wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kuanzia mwaka 2025 hadi mwaka 2026.