Taasisi ya Utafiti ya CMG yazinduliwa rasmi hapa Beijing
2024-06-07 15:02:51| cri

Taasisi ya Utafiti ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) imezinduliwa rasmi leo Juni 7 hapa Beijing. Naibu mkurugenzi wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong, mkuu wa Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China na mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Historia ya China Bw. Gao Xiang wamehudhuria halfa ya uzinduzi wa taasisi hiyo.

Taasisi hiyo itakusanya raslimali na vipaji vya hali ya juu duniani kwa njia za kivumbuzi, na kujenga jukwaa jumuishi la utafiti wa nadharia, ukuzaji wa vipaji na mazoezi ya kiutendaji, ili kuiwezesha CMG ibebe majukumu mapya na kupata mafanikio mapya katika kusaidia kutimiza azma ya Chama na Nchi.