Mila potofu zinavyowaathiri watoto wa kike na wanawake
2024-06-08 09:00:41| CRI


 Tarehe 16 Juni kila mwaka ni Siku ya Mtoto wa Afrika. Siku hii ilianzishwa mwaka 1991 na Umoja wa Afrika (AU) wakati huo ukijulikana kama Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU) ili kuwaenzi wanafunzi weusi nchini Afrika waliouliwa mwaka 1976 wakati wakipinga utawala wa ubaguzi wa rangi na sera zake za elimu. Tangu wakati huo siku hii maalum inakusudia kuongeza ufahamu kuhusu changamoto na fursa ambazo watoto wa Afrika wanakabiliwa nazo, hasa katika maeneo ya afya, elimu, na ulinzi.

Sasa tukiwa tunaelekea katika Siku hiyo muhimu kwa bara la Afrika, kuna baadhi ya mila na desturi ambazo zimekuwa ni kipingamizi kwa mtoto wa kike na mwanamke kufikia ama kutimiza ndoto zake. Kuna mila na desturi nyingi ambazo zimepitwa na wakati na hazipaswi kufuatwa katika dunia ya sasa. Hivyo katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tunaangazia baadhi ya mila na desturi hizo.