Wakimbizi zaidi ya milioni moja wa Burundi nchini Tanzania warejeshwa makwao
2024-06-10 08:56:16| CRI

Katibu mtendaji wa kudumu katika Wizara ya Mambo ya Ndani, Maendeleo ya Jamii, na Usalama wa Umma wa Burundi Theophile Ndarufatiye amesema, wakimbizi takriban milioni 1.1 wa Burundi wanaoishi katika kambi za wakimbizi magharibi mwa Tanzania wamerejeshwa kwa hiari nchini mwao tangu mwaka 2017.

Ndarufatiye amesema wakimbizi laki moja wa Burundi bado wanaishi katika kambi za wakimbizi za Nduta na Nyarugusu katika mkoa wa Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Ndarufatiye amesema hayo katika mkutano na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Hamad Masauni, ambao pia ulihudhuriwa na maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, (UNHCR).

Viongozi hao wawili walikubaliana kuwa wakimbizi wa Burundi waliosalia nchini Tanzania watarejeshwa kwa hiari nchini kwao kabla ya tarehe 31 Desemba mwaka 2024.

Ndarufatiye ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi wa Burundi kwa muda mrefu.